Maskini ya mungu!Jamaa kakatwa nanihii live !..
Mwanamama mmoja nchini Bangladeshi ameukata uume wa mwanaume mmoja-- - na kuupeleka polisi kama ushahidi kuwa alikuwa akitaka kubakwa. Kwa mujibu wa mtandao wa BBC mwanamama huyo mwenye umri wa miaka arobaini alifanya hivyo siku ya Jumatatu.
Mwanamama huyo ambaye ameolewa na ana watoto watatu, amedai kuwa alishambuliwa wakati akiwa amelala katika wilaya ya Jhalakathi, karibu kilomita mia mbili kusini mwa mji mkuu Dhaka.
Maafisa wa polisi wanasema mwanaume anayetuhumiwa kutaka kumbaka pia ana miaka arobaini na ana watoto watano. "Wakati akijaribu kumbaka, mwanamke huyo alimkata kwa kutumia kisu, halafu akaifunga kwenye mfuko wa karatasi na kuileta polisi kama ushahidi" amesema Abdul Khaer, mkuu wa polisi wa huko.
Kipande hicho kilichokatwa kiliachwa polisi wakati mshukiwa huyo akitibiwa hospitali. Hata hivyo mtuhumiwa huyo anasema mwanamama huyo alikuwa mpenzi wake, na alimtaka watoroke wakaishi pamoja.
Bwana huyo amesema alipokataa ombi la mwanamke huyo, ndipo alishambuliwa. Mkuu wa polisi Khaer amesema watamkamata, mara tu atakapopata nafuu. Daktari wa hospitali anapotibiwa mtuhumiwa huyo amesema imeshindikana kuunganisha kipande kilichokatwa.
Na kwa taarifa yako,
... Ukifika umri wa miaka 75, utakuwa umelala kwa takriban miaka 23 kwa jumla...
edwin Ze great